Jumapili , 23rd Aug , 2015

Kocha wa Timu ya Ruvu Shooting Tom Olaba amesema kiwango kinachooneshwa na timu yake bado hajaridhishwa nacho kwani anahitaji kufika mbali zaidi ya alipo sasa.

Katika taarifa yake, Olaba amesema, licha ya kikosi chake kufanya vizuri katika mechi za kirafiki lakini anafanya bidii ili kikosi chake kufikia ubora wanaouhitaji ili kufika mbali zaidi kuliko timu yoyote inayoshiriki michuano ya ligi daraja la kwanza.

Kocha Olaba amesema, timu hiyo imeshuka daraja jambo lililowashtua mashabiki wa timu hiyo lakini anaamini timu hiyo itarudi katika kiwango chake cha awali na itaendeleza ushindani katika ligi hapa nchini.