Alhamisi , 23rd Jul , 2020

Klabu ya soka ya Villarreal ,imethibitisha kukamilisha usajili wa aliyekua kocha wa klabu ya Arsenal, Unai Emery ambaye amesaini mkataba wa miaka mitatu.

Kocha wa zamani wa klabu za Sevilla,PSG na Arsenal (Pichani) akiwa katika majukumu yake.

Raia huyo wa Hispania ambaye alifutwa kazi na Arsenal mwezi novemba mwaka jana baada ya kudumu na The Gunners kwa miezi 18, ametua Villarreal kutwaa mikoba ya Javi Calleja aliyetimuliwa.

Unai ambaye aliwa kuifundisha PSG ya Ufaransa, anarejea Hipsania ambapo alianzia kazi hapo kuzifundisha timu za Valencia na Sevilla ambayo ailiiwezesha kutwaa taji la Ulaya ngazi ya vilabu mara tatu mfululizo katika miaka ya 2014, 2015 na 2016.

Kocha huyo aliivisaidia vilabu vya hivyo kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya, pia kuiwezesha Valencia kumaliza nafasi ya tatu katika La Liga mara tatu wakati Sevilla ilitikisa katika Europa.