Jumatatu , 14th Nov , 2016

Timu ya Azam FC inatarajia kucheza mchezo wake wa kirafiki dhidi ya Ruvu Shooting leo usiku ikiwa ni nafasi ya benchi la ufundi kufanyia tathmini kikosi hicho kabla ya kuongeza nguvu mpya kwenye usajili wa dirisha dogo.

Azam katika majaribio

 

Afisa habari wa Azam FC Jaffary Iddy Maganga amesema, Azam FC imepokea jumla ya wachezaji saba kutoka Cameroon, Ghana na Ivory Coast ambao walianza kujaribiwa kwenye mchezo wa Jumamosi uliopita dhidi ya JKT Ruvu na Azam kupoteza kwa mabao 2-0 na mchezo wa leo ndiyo utaamua nani anafaa ndani ya kikosi hicho.

Maganga amesema, mara baada ya mchezo huo kocha Zeben Hernandez atawasilisha ripoti ya jumla kabla ya kuvunja kambi mpaka Desemba 3, mwaka huu ambapo wataanza maandalizi ya mzunguko wa pili.

Nyota hao ni mabeki Mbimbe Nkot (Cameroon), Kone Nabil Ibrahim (Ivory Coast) na kiungo Mpondo Stephane wa Cameroon huku washambuliaji wakiwa ni Yaya Awaba Joel (Cameroon), Konan Oussou (Ivory Coast) na Waghana Samuel Afull na Benard Offori.