Jumanne , 10th Oct , 2017

Kuelekea raundi ya sita ligi kuu ya soka nchini VPL wikiendi ijayo, kikosi cha Azam FC kimeondoka jijini Dar es salaam kuelekea Shinyanga kwaajili ya mchezo wake dhidi ya Mwadui FC.

Taarifa kutoka klabu ya Azam FC imesema klabu hiyo itatua Shinyanga siku ya Jumatano ambapo leo itapumzika mkoani Dodoma kisha kuendelea na safari siku ya kesho.

Azam FC imeondoka na kikosi kamili isipokuwa kiungo Stephan Kingue, ambaye bado hajapona vizuri majeraha yake ya mgongo.

Ikiwa Kanda ya ziwa Azam itacheza michezo miwili Oktoba 14 dhidi ya Mwadui FC pamoja na ule wa Oktoba 21 dhidi ya Mbao FC utakaopigwa jijini Mwanza.

Kwenye msimamo wa ligi Azam FC inashika nafasi ya tatu ikiwa na alama 11 wakati wenyeji wao Mwadui FC wana alama 4 katika nafasi ya 12. Mbao FC ipo nafasi ya 9 ikiwa na alama 5.