Alhamisi , 10th Apr , 2014

Kikosi cha Azam kimepata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Ruvu Shooting na kufikisha point 56 ikiwa ni point 4 mbele ya Yanga yenye point 52 na hivyo kuukaribia ubingwa wa ligi kuu Tanzania Bara kwa kuhitaji point 3 pekee.

Kikosi cha Azam kikijifua katika uwanja wake wa nyumbani

Ligi kuu ya Tazania bara imeendelea leo kwa mchezo mmoja uliopigwa katika dimba la mabatini Mlandizi mkoani Pwani ikiwakutanisha Azam na Ruvu Shooting.
Mechi hiyo imechezwa leo baada ya hapo jana kuahirishwa kutokana na mvua kubwa iliyosababisha uwanja kujaa maji.
Matokeo katika mchezo huo ni kwamba Azam imepata ushindi wa mabao 3 kwa 0 yaliyotiwa wavuni na Gaudence Mwaikimba, Himid Mao na kipre Tchetche.
Kwa matokeo haya Azam imeendelea kuongoza ligi kwa kuwa na point 56 ikifuatiwa na Yanga yenye point 52.
Sasa Azam itahitaji point 3 pekee kutangazwa mabingwa wapya wa ligi hii kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwake na imebakiwa na michezo miwili ambayo ni kati yake na Mbeya City pamoja na mchezo dhidi ya JKT Ruvu.