
Akiongea leo Jaffary amesema kijana huyo amekuwa na mwendelezo wa kufanya vizuri tangu apewe nafasi katika kikosi cha kwanza akitokea timu ya vijana chini ya miaka 20.
''Paul Peter juzi tu amefunga mabao matatu baada ya kuingia kipindi cha pili kwenye mchezo dhidi ya Shupavu FC na pia sio hapo tu alifunga bao la kusawazisha dhidi ya Singida United kwenye mchezo wa ligi, kwahiyo unaweza kuona ni mchezaji wa aina gani'', amesema.
Paul Peter jana amesaini mkataba wa miaka minne ambao utamfanya aitumikie klabu hiyo kwenye kikosi cha timu A, ambapo Jaffary ameongeza kuwa uongozi wa timu hiyo una matumaini kuwa kijana huyo ataendelea kuwa suluhisho la magoli kwenye timu.
Paul alianza kuwa gumzo nchini baada ya kusawazisha bao katika dakika za mwisho kwenye mchezo wa ligi kati ya Azam FC na Singida United kabla ya kufunga mabao matatu (Hat-trick) kwenye mchezo wa kombe la shirikisho dhidi ya Shupavu FC. Mechi zote aliingia kipindi cha pili.