Jumanne , 11th Jun , 2024

Uongozi wa Azam FC umethibitisha rasmi kujiondoa kushiriki michuano ya CECAFA Kagame Cup 2024 ambayo inatarajiwa kuanza rasmi mnamo Julai 6 mpaka 22-2024 kwenye shindano litakalofanyika Tanzania Bara pamoja Zanzibar.

Akizungumza kwenye mahojiano maalum na EATV,Meneja  Habari na Mawasiliano wa Azam FC Thabit Zakaria amesema kutokana na uwepo wa ratiba ngumu inayowakabili kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya wa mashindano 2024-25 watashindwa kujiandaa kikamilifu kuelekea shindano la msimu huu.

''Tarehe hizo zitakuwa ngumu kwetu kutokana na wachezaji  wote wanatakiwa kukaa press session zaidi ya wiki sita na hii kwa mujibu wa kitalaamu  timu iwe tayari kwa mashindano ''amesema Meneja habari Azam FC  Zaka Zakazi. FC.

Kwa upande mwingine,Thabit Zakaria maarufu kama  Zaka Zakazi amesema bado wanaendelea kuboresha kikosi chao kwa kufanya usajili wenye tija katika kuwasaidia kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali wanayokwenda kushiriki kwa msimu 2024-25.

Azam FC iliyomaliza nafasi ya pili ndani ya ligi kuu Tanzania Bara msimu 2023-24 inajiandaa kushiriki kwenye ligi ya mabingwa barani Afrika msimu 2024-25.