Jumatano , 6th Apr , 2022

Kocha mkuu wa FC Barcelona Xavi Hernandez amesifia usajili wa nyota Pierre Emerick Aubameyang ndani ya viunga vya Camp Nou baada ya nyota huyo kufunga magoli 9 kwenye michezo 12 tangu asajiliwe kwenye dirisha dogo la January akitokea klabu ya Arsenal ya England.

(Nyota wa Fc Barcelona Pierre Emerick Aubameyang )

"kuwa na Auba ni zawadi kutoka mbinguni, ni fahari kuwa na mchezaji kama yeye ambaye anatoa mchango mkubwa kwenye timu". Amesema Xavi huku akiungwa mkono na nahodha wa klabu hiyo Sergio Busquets

"alipokuja kujiunga na timu alihitaji muda mwingi wa kucheza na hapa anapata  , natumaini atakuwa na muendelezo uliokuwa mzuri zaidi na sisi kumpata kama mchezaji huru ni zawadi tosha kwetu”amesema Busquets

Mkataba wa nyota huyo utamalizika mwaka 2025 huku Barcelona siku ya Alhamisi watacheza na klabu ya Frankfurt ya Ujerumani kwenye mchezo wa robo fainali ya michuano ya Europa league na wakifuzu hatua hiyo watapambana na mshindi kati ya Lyon au West Ham United kwenye hatua ya nusu fainali .