Kipa wa Timu ya Simba SC, Vicent Angban akipeana nkono na kipa wa Yanga, Ally Mustafa
Angban alitakiwa kutua nchini Jumapili iliyopita akiambatana na mshambuliaji raia mwenzake wa Ivory Coast ambaye anatarajiwa kusajiliwa na Simba, Blagnon Goue Fredric, lakini alishindwa kufanya hivyo baada ya kudaiwa kuchelewa ndege.
Hata hivyo, Fredric ambaye ni mshambuliaji yeye alitua peke yake siku hiyo ya Jumapili na kupokelewa na viongozi wa timu hiyo ambao tayari wanadaiwa kufanya naye mazungumzo ya awali na kinachosubiriwa sasa ni kuangaliwa uwezo wake na Omog ndipo aweze kusajiliwa.
Meneja wa Simba Abassi Ally alisema kuwa Angban ametua juzi Jumatatu na kwenda moja kwa moja kuonana na viongozi wa timu hiyo.




