Jumanne , 18th Feb , 2025

Kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti amesema kauli ya  Pep Guardiola ni mbinu maalumu za kuwatoa mambingwa hao watetezi wa UCL mchezoni kuelekea katika mchezo wa marudiano utakaopigwa kesho katika uwanja wa Santiago Bernabeu  

Carlo Ancelotti - Kocha wa Real Madrid

Pep Guardiola Baada ya ushindi wa 4-0 dhidi ya Newcastle United siku ya Jumamosi alisema Manchester City ina  asilimia moja tu  katika nafasi  ya kufuzu hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya

Ikumbukwe Real  Madrid wanaongoza kwa mabao 3-2 dhidi ya Man City  ambao wanashika nafasi ya nne katika msimamo wa EPL