Alhamisi , 7th Mar , 2019

Kocha mkuu wa klabu ya soka ya Yanga, Mwinyi Zahera ameingilia kati uvumi uliopo kuwa pesa zinazotolewa na wanachama kwaajili ya kusaidia klabu zinapigwa na viongozi, huku akiweka wazi kuwa hakuna jambo kama hilo.

Kocha wa Yanga kushoto na Ajibu kulia.

Zahera amesema kuwa hayo maneno sio ya kweli kwasababu pesa zote zinazoingia wanashirikishwa matumizi yake.

''Kuna watu wanashambaza hizi taarifa ili wanachama wetu wasichangie, timu yao ipate matatizo lakini kiukweli hakuna hata elfu moja ambayo imeibiwa zote zinatumiaka vizuri na wala viongozi hawazichukui'', amesema.

Kwa upande wake nahodha Ibrahim Ajibu yeye amesema kuwa ni shuhuda namba moja wa matumizi ya pesa hivyo kwani kila pesa inayotoka ni lazima waidhinishe yeye na kocha hivyo hakuna ukweli kuwa pesa hizo zinaibiwa.