Jumatano , 17th Jul , 2024

Nyota Mtanzania Aisha Masaka amejiunga rasmi leo Julai 17-2024 na klabu ya Wanawake ya Brighton & Hove Albion inayoshiriki Ligi Kuu ya Wanawake nchini Uingereza akitokea timu ya BK Hacken ya Sweden kwa ada ya uhamisho ambayo haijawekwa wazi

Mkurugenzi wa Michezo kwa soka la Wanawake Brighton & Hove Albion  Zoe Johson amesema tunafuraha ya kumkaribisha Aisha ndani ya Brighton, Amekuwa na msimu mzuri na mwenye muendelezo mkubwa akiwa Sweden  akiiwakilisha Hacken kwenye ligi ya mabingwa  barani Ulaya 2023-24”.

Aisha Masaka mwenye umri wa miaka 20 alijiunga na Hacken  mnamo mwaka 2022 akitokea klabu ya Yanga  ambapo  kabla ya hapo aliwahi  kuichezea timu ya Alliance FC Mwanza huku mpaka sasa ameichezea timu ya Tanzania “Twiga Stars ” kwenye michezo 15 tangu mwaka 2021