Aguero azidi kuziumiza kichwa timu zinazomuhitaji

Jumapili , 2nd Mei , 2021

Klabu ya Everton wamejiunga kwenye mbio za kumsajili mshambuliaji wa Manchester City Sergio Kun Aguero katika majira ya joto mwaka huu,

Mshambuliaji mahiri wa Manchester City Sergio kun Aguero

“The Toffees” wamemuahidi mshambuliaji huyo dau kubwa la usajili ili kuvipiku vilabu vya Barcelona, Inter Milan, Chelsea, Tottenham na Leeds United ambao nao wameonyesha kumuhitaji mchezaji huyo.

Everton ndio timu pekee iliyojiunga hivi karibuni katika kuwania sahihi ya Aguero wakati atakapoondoka Manchester City majira haya ya joto mwaka huu.

Mshambuliaji huyo raia wa Argentina mwenye umri wa miaka 32, anamaliza mkataba wake na matajiri hao wa jiji la Manchester mwishoni mwa msimu huu, kwa hivyo atakua huru na kupatikana kwa uhamisho wa bure baada ya kuhudumu katika dimba la Etihad kwa takriban miaka kumi.