Jumatatu , 28th Jan , 2019

Shirikisho la soka barani Afrika (CAF), limetangaza kusogeza mbele kwa wiki moja michuano ya AFCON 2019 kutoka kuanza Juni 14 na kumalizika Julai 13 kama ilivyopangwa awali.

Cameroon walipotwaa ubingwa wa AFCON 2017

Kwa mujibu wa taarifa ya CAF imesema kuwa michuano hiyo sasa itaanza Juni 21 na kumalizika Julai 13, 2019 huku nchi mwenyeji ikiendelea kuwa ni Misri.

Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa droo ya kupanga makundi itafanyika Ijumaa ya April 12, 2019.

Sababu kubwa ya kubadilisha tarehe ya michuano hiyo ni baada ya Shirikisho hilo kutaarifiwa na waandaaji wa michuano hiyo, Misri, kwamba tarehe iliyopangwa awali inaingiliana na mwezi mtukufu wa Ramadhan hivyo inaweza kuathiri viwango vya wachezaji wa wenye imani ya Kiislam.

Misri ilipata haki ya kuandaa michuano hiyo baada ya waandaaji wa awali, Cameroon kushindwa kuiridhisha CAF kwa maandalizi yake.