Jumatano , 15th Sep , 2021

Baada ya kukosa michuano ya Ligi ya mabingwa Barani ulaya kwa takribani miaka saba, miamba ya soka kutoka nchini Italia, AC Milan watakuwa na kibaru kizito dhidi Liverpool, usiku wa leo katika mchezo wa kwanza wa kundi B kwenye michuano hiyo.

Baadhi ya wachezaji wa AC Milan wakishangilia baada ya kufunga bao kwenye moja ya mchezo wa ligi kuu Italia 'Serie A'.

Mchezo huo ambao ni kumbukizi ya fainali ya mwaka 2005, Liverppol wakitwaa ufalme wa Ulaya na 2007 ulimwengu uliposhuhudia Milan wakilipa kisasi. 

Mtanange wa leo, historia itakuwa haina nafasi yoyote kwa pande zote mbili kutokana na mabadiliko,  utofauti na ubora kati ya vikosi hivyo, huku Liverpool ikipewa nafasi kubwa kushinda.

AC Milan watamkosa mkongwe Zlatan Ibrahimovic, lakini uwepo wa wachezaji wenye uwezo na vipaji kama  Theo Hernandez, Fikayo Tomori, Olivier Giroud, Sandro Tonali, Franck Kessie, Rafael Leao, Ante Rebic, Brahim Diaz, utampa unafuu kupanga Kocha Stefano Pioli.