Jumatatu , 18th Mei , 2015

Wachezaji 35 wa timu ya Taifa ya Mpira wa Netiboli wanatarajiwa kuingia kambi ya awali hapo kesho visiwani Zanzibar.

Akizungumza na East Africa Radio, mwenyekiti wa chama cha Netiboli Tanzania CHANETA, Anna Kibira amesema, kambi hiyo itakuwa na awamu nne Bara na visiwani pamoja na kucheza michezo ya kirafiki kabla ya kupatikana kwa wachezaji 12 watakaoshiriki michuano ya Afrika itakayofanyika Juni mwaka huu nchini Namibia.

Kibira amesema, baada ya kupata wachezaji 12 watakaokuwa katika kambi hiyo hadi awamu ya mwisho, wataondoka Juni 26 mwaka huu kuelekea nchini Namibia kwa ajili ya maandalizi ya kuiwakilisha nchi katika michuano hiyo ya Afrika.