Jumatano , 1st Nov , 2023

Kwa siku za hivi karibuni kumeibuka utaratibu mpya ambao idadi kubwa ya watumiaji wa mtandao wa ''YouTube'' wamekuwa wakiutumia,

Utaratibu wenyewe unafahamika kama ''Ads Block'' kizuizi cha matangazo,

 

Kwa wengi wetu tunaweza kuwa mashuhuda wa yale matangazo ambayo yanakuwako mwanzo kati na mwisho mwa-video husika, kwenye mtandao wa YouTube

Lakini huwenda ukawa ni miongoni mwa mamia ya watu ambao huchukizwa na matangazo hayo,

Lakini ulikosa namna ya kufanya kwani kiwango cha pesa ambacho kilihitajika ulipie ili matangazo hayo yasiwepo wakati unatazama video YouTube huwenda kilikuwa kikubwa kwa upande wako,

Ndipo hapo likaja wazo la kuzuia matangazo ''Ads Block'' lakini hapa nako kuna makundi wapo wanaozuia kupitia kisakuzi husika kwa maana ya ''Browser'' mfano Google Chrome na wapo pia wanaozui kupitia ''Application'' maalumu.

Sasa kutokana na mlolongo wa haya yote 

Taarifa mpya kutokea kampuni ya YouTube ni kwamba wameamua kuonyesha makali kwa wale wote wanaotumia ''Ads Block'' vizuizi vya matangazo, watumiapo mtandao huo.

Kwani kufanya hivyo ni kukiuka masharti yaliyoweka na mtandao huo kimatumizi, na utaratibu ulivyo ili utazame ikiwa kama hujalipia YouTube premium basi matangazo lazima uyaone.

Kwenye mazungumzo na wavuti ya ''The Verge'' YouTube wamethibitisha ya kwamba kwa sasa wanapanga kuja na utaratibu kwa watumiaji wote, kuwauliza iwapo watachagua kulipia ''YouTube Premium'' au waendelee kuruhusu matangazo ndani ya mtandao huo. 

Na sote tunafahamu kuwa hakuna ambaye anatamani kufanya biashara ambayo haimuingizi pesa au faida, hivyo upo wasiwasi ya kuwa wapeleka matangazo kwenye mtandao huo wamepunguwa kwa sababu ya ongezeko kubwa la watu wanazuia matangazo.

Picha: digitalchaoscontrol.com