Ijumaa , 3rd Apr , 2020

Wanaume wawili kutoka Mtaa wa Oljorai eneo la Gilgil, Kaunti ya Nakuru nchini Kenya, wameuana kwa kukatana mapanga kisa kupigania mwanamke.

Gari la polisi likiendelea na uchunguzi wa tukio hilo

 

Wanaume hao wanadaiwa kuwa na umri wa miaka 40 kwa kila mmoja, walikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanmke huyo kwa muda wa miaka miwili bila ya wao kujuana.

Akithibitisha kisa hicho Kamishna wa Polisi kaunti ya Gilgil, Ndambuki Mutheki,amesema wawili hao wameshambuliana kwa mapanga, mmoja amekatwa maeneo ya shingoni mwingine amefariki njiani wakati anakimbizwa hospitali.

Kwa upande wa mashuda wa eneo hilo wamesema, mwanamke huyo alikuwa na watoto watatu ambao baba yao hajulikani, na chanzo cha kutokea kwa tukio hilo ni mmoja wa wanaume hao kumtembelea mwanmke huyo na kumkuta mwenzake anaandaliwa chai majira ya asubuhi.

Baada ya hapo wakaanza kubishana kwa maneno kisha kushambuliana kwa mapanga.