
Picha ya Ng'ombe
Kulingana na taarifa ya mkazi mmoja amesema uhaba wa maji katika eneo hilo ndiyo umewafanya wakazi kutumia njia hiyo ili kuzuia kusambaa kwa virusi hivyo.
Aidha mmoja wa mfugaji katika eneo hilo aitwaye Lokoliok Losike amesema anaamini kuwa mkojo wa ng'ombe unasaidia katika kuzuia maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa COVID-19.
Pia Wizara ya Afya katika kaunti hiyo imewataka wakazi waishio eneo hilo kuosha mikono kila wakati na kuvaaa barakoa "maski" kila wanapaokuwa na mikusanyiko na watu wengine.
Chanzo : Tuko News