Jumatatu , 6th Apr , 2020

Nchi ya India imesitisha safari za usafiri wa Treni kupitia Shirika lake la Indian Railways, badala yake watatumia kama hospitali za muda kwa ajili ya uangalizi na matibabu ya mlipuko wa ugonjwa wa Virusi vya Corona.

Mabehewa yaliogeuzwa kuwa Hospitali kwa muda kwa ajili ya Ugonjwa wa Corona nchini India

Shirika la reli nchini India linashika nafasi ya nne kati ya mashirika makubwa ya usafiri huo duniani, na kwa mara ya kwanza wametangaza kufunga kufanya shughuli hizo baada ya kupita miaka 167.

Waziri Mkuu wa Taifa hilo Narendra Modi, alitangaza watu kutotoka nje siku ya Machi 25 na shirika hilo lilipewa muda wa kusafirisha abiria wanaotumia usafiri huo hadi Aprili 14, ila wamesitisha kutokana na ugonjwa huo kusambaa kwa wingi nchini humo.

Siku ya Aprili 1 nchi ya India iliweka rekodi ya kutangaza kesi 4,288 ya Virusi vya ugonjwa wa Corona na vifo 117 vya ugonjwa huo.