Alhamisi , 30th Dec , 2021

Mtaalam wa masuala ya mahusiano na saikolojia, Jiwa Hassan, amewashauri watu wasiwe wepesi wa kubadili dini kwa kigezo cha kuolewa ama kuoa, kwa sababu unaweza kuachika na kushindwa kurudia dini yako ya zamani na utaonekana unamtania Mungu.

Mtaalam wa masuala ya mahusiano na saikolojia, Jiwa Hassan

Kauli hiyo ameitoa hii leo Desemba 30, 2021, wakati akizungumza kwenye kipindi cha SupaBreakfast cha East Africa Radio, na kusisitiza kwamba watu wanapaswa kubadili dini kwa sababu tu unampenda Mungu na kupenda mafunzo ya huko.

"Mara nyingi kubadili dini ili uolewe ama uoe si kigezo kizuri kwa sababu utaachika na hauwezi kurudi kwenye dini yako ya zamani utaonekana unamtania Mungu, nenda kwenye dini nyingine sababu unampenda Mungu na mafunzo ya huko," amesema Jiwa Hassan