
Wanamitindo waliojitokeza.
Wakiongea wakati wa zoezi hilo la usahili baadhi ya wanamitindo wapya wamesema kwa sasa kazi ya uanamitindo ni ajira ambayo imeinua kipato cha vijana wengi nchini huku wakiwashukuru waandaji na wadhamini wa tamasha hilo ikiwemo kampuni ya East Africa Television Limited.
Kwa upande wao waandaji na majaji wa tamasha hilo wamesema wingi wa washiriki waliojitokeza umeonesha dhahiri jamii umuhimu wa tasnia hii ya mitindo ambayo huko nyuma ilikuwa na changamoto kubwa.
Tamasha la mitindo la TAFF linalosubiriwa kwa hamu kubwa na wakazi wa Jijini Dar es Salaam na vitongoji vyake linafanyika wakati huu wa majira ya joto, Terrace Slip Way Masaki kando ya swimming pool ili watu waweze kupata upepo mwanana wakijionea mitindo mbalimbali.