Jumanne , 7th Jun , 2022

Kupitia kipindi cha Mama Mia, Rais wa Rotary Club of Dar es Salaam, Aisha Sykes ameelezea namna walivyoguswa na kampeni ya Namthamini na kuamua kujitolea taulo za kike kwa ajili ya kuhakikisha mtoto wa kike anaendelea na masomo yake pale anapokuwa kwenye siku zake za hedhi.

Rais wa Rotary Club of Dar es Salaam, Aisha Sykes.

"Tumeguswa kwa sababu sisi Rotary kazi zetu ni za kujitolea, tukiangalia wapi kwenye jamii kuna changamoto. Nilivyoisikia hii kampeni ya Namthamini nikasema East Africa Radio mmekuwa mnatupa support Rotary miaka yote, leo na nyinyi mna kampeni ambayo imetugusa sisi, tuliona ni muhimu kwa ajili ya kuwaunga mkono kuwasaidia watoto wa kike waondokane na changamoto" - Aisha Sykes.

Rotary Club wapo pamoja na kampeni ya Namthamini kwa mwaka 2022 tangu ilipozinduliwa Mei 27 mwaka huu katika shule ya sekondari Kidete, Kigamboni.

Kampeni ya Namthamini Wilaya ya Kigamboni ilihusisha shule mbili za Sekondari Kidete na Kibugumo. Jumla ya Pakiti 3572 za taulo za kike ziligawanywa kwa shule hizo mbili, kila shule ilipata pakiti 1786.