
Ritha Chuwalo baada ya kupokea cheti cha mafunzo kutoka taasisi ya AVAC
Baada ya kumaliza mafunzo ya kuripoti magonjwa ya mlipuko pamoja na chanjo yaliyotolewa kwa siku tatu na taasisi hiyo jijini Nairobi, Kenya.
Baada ya kupokea cheti hicho Ritha kupokea ukurasa wake wa instagram ameandika
''Naishukuru Taasisi ya AVAC ya Nchini Marekani kwa kufadhili mafunzo haya kwa jamii mbalimbali za watu wa Afrika kupitia sisi waandishi wa habari ambako magonjwa ya mlipuko ni janga kubwa kutokana na mazingira wanayotoka.
Pili nawashukuru tena na tena Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania TAMWA kwa kunipendekeza kushiriki mafunzo haya na tatu na mwisho lakini sio kwa umuhimu ni Uongozi mzima wa EATV Company Limited kwa kunipa kibali kuhudhuria mafunzo haya .