Jumapili , 19th Jun , 2022

Rais wa Rotary Club Duniani, Shekher Mehta amefanya ziara katika hospitali ya Muhimbili wodi ya watoto wanaougua saratani mbalimbali ambayo taasisi hiyo imechangia na inaendelea kuchangia huduma mbalimbali.

Rais wa Rotary Club duniani, Shekher Mehta akiwasili hospitali ya Muhimbili

Akitoa maelezo ya kinachofanyika katika wodi hiyo Afisa Mtendaji wa taasisi ya Tumaini la Maisha, Dr.Trish Scanlan amesema Rotary club, Hospitali ya Taifa Muhimbili na taasisi yake wanafanya kazi pamoja ya kuhakikisha watoto wanaougua saratani wanapatiwa tiba.

Wodi hiyo ya watoto wanaougua saratani ina vitanda 65, na kwa upande hosteli kuna vitanda 22, jumla ni 87 ambapo vyote hujaa na kuna wakati idadi inaongezeka. Saratani zinazoongoza kuwapata watoto ni saratani ya macho, matezi na tumbo.