
Askofu Wiliam Mwamalanga
Askofu William Mwamalanga amesema siku ya Pasaka Mungu amedhibitisha kuwa binaadam si lolote wala chochote kwenye dunia hii.
"Pasaka ya mwaka huu itakuwa na maana kubwa sana kwa watanzania, Pasaka sio kula pilau, kutafuta bia na ulevi vitu hivyo ni kinyume, maana ya Pasaka ni kutulia na kujifunza maana Mungu anadhibitisha kwamba binaadam si lolote na si chochote na unaishi kwa maisha ambayo umeyaazima, tofauti na Yesu alivyosema nitakufa na siku ya tatu nitafufuka" ameeleza Askofu William Mwamalanga