
Picha ya msanii Nay Wa Mitego
Akizungumza na EATV & EA Radio Digital, Nay Wa Mitego amesema hakuna mahali popote wanaposema kama utafuatili dini utaenda mbinguni.
"Imani yangu ni ya tofauti sana, sina dini wala kabila kwanza dini itakupeleka wapi, hakuna sehemu iliyoandikwa kwamba itakupeleka mbinguni, halafu tuamini katika dini gani sasa Uislam au Ukristo na ipi ndiyo sahihi, mimi naamini katika imani yangu ya Mungu hata vitabu vya dini vimeandika hivyo" amesema Nay Wa Mitego.