Jumanne , 7th Apr , 2020

Taarifa njema kutoka nchini Italia zinadai, mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 104, ameweka rekodi mpya ya kupata maendeleo mazuri ya kiafya baada ya kupambana na ugonjwa unaosabbaishwa na Virusi vya Corona.

Mzee wa miaka 103 upande wa kulia ambaye amepona Corona

Mzee huyo aitwaye Ada Zanusso alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa unaosababishwa na Virusi vya Corona, amepata ahueni wakati akipatiwa matibabu nyumbani kwake Biella Kaskazini mwa nchi ya Italia.

Akitoa dalili za kuhusu ugonjwa huo mzee huyo amesema alikuwa anatapika, homa, kupata ugumu wa kupumua, na alivyofanya vipimo akakutwa na virusi vya Corona.

Aidha Daktari ambaye alikuwa anampa matibabu amesema kuwa, "Ameweza kuamka kutoka kitandani wala sio uongo na anaweza kutembea kwenda kwenye kiti chake, kuendelea kwake vizuri ni furaha kwetu na inatupa matumaini kwa wote wanaoumwa kwa wakati huu mgumu"

Ana Zanusso amevunja rekodi ya Mr P mwenye miaka 101, kuwa mtu wa kwanza mwenye umri mrefu kupona ugonjwa wa Corona nchini Italia.

Pia mwanamke mwingine ambaye jina lake limehifadhiwa  kutoka nchini Iran mwenye miaka 103, naye amepona Corona baada ya kuumwa kwa siku tatu.