
Picha ya waandamanaji
Afisa polisi Derek Chauvin (45) alipigwa picha wakati akiwa amemkandamiza kwa kutumia goti kwenye shingo Floyd kwa zaidi ya dakika tisa wakati wa kukamatwa kwake.
Kifo chake kilizua maandamano makubwa Marekani hadi kusababisha kuanzishwa kwa harakati za mapambano (Black Lives Matter) ulimwenguni kote ya kuleta mazungumzo juu ya mbio za mageuzi ya polisi dhidi ya ukatili kwa watu weusi.
Aprili 20,2021 Mahakama ilimkuta na hatia ya mauaji, Derek Chauvin na hukumu ya kesi yake inatarajiwa kutoka mwezi ujao.