Alhamisi , 9th Jun , 2022

Meneja wa mwanamziki Steve Rnb, Amri The Business siku ya leo amechangia boksi moja la taulo za kike kwa ajili ya kusaidia wanafunzi wa kike mashuleni kupitia kampeni ya Namthamini ambapo mchango huo utaweza kusaidia wanafunzi wawili shuleni kwa mwaka mzima.

Amri akikabidhi mchango wake katika ofisi za East Africa TV, Mikocheni.

Amri anasema ametoa mchango huo kwa sababu anatambua changamoto wanazopitia watoto wa kike wanapokuwa katika kipindi cha hedhi.

Kila mmoja anakaribishwa katika ofisi zetu za East Africa TV zilizopo ITV Mikocheni, Dar es salaam kuchangia kwa namna ambavyo utaweza, ambapo unaweza kuwasilisha mchango wako wa taulo za kike au fedha bila kujali ni kiasi gani.