Msanii wa Injili Christina Shusho
Akizungumza kwenye show maalum ya Friday Night Live Christina Shusho amesema
"Kikubwa ninachokikumbuka wakati wa uongozi wake kwa mara ya kwanza nikaanza kupiga kura kumbukumbu hiyo hainitoki nashukuru Mungu ni baraka, amefanya vizuri na tuna mengi ya kujifunza kutoka kwake, nakumbuka tena mwaka 1999 anatangaza kifo cha Baba wa Taifa kwa wakati huo ilikuwa ngumu kwa sababu tulikuwa tuna hofu ya kuingia mwaka 2000 maana tuliambiwa Yesu anarudi kutakuwa na mabomu, mlipuko na radi" ameeleza Christina Shusho
Zaidi tazama kwenye video hapa chini