Jumatatu , 24th Apr , 2023

Video ya mchungaji mmoja kutoka nchini Nigeria imesambaa mitandaoni akiamuru simu za waumini wake ambazo hazikuwa na chaji, ibada itakapomalizika zitakuwa zimeingia chaji kupitia muujiza, huku muumini mmoja akitoa ushuhuda simu yake ilianza kuchaji ibada tu ilipoanza.

Kushoto ni Mchungaji mtangaza muujiza

Kupitia videoyako hiyo mtandaoni, mchunga kondoo huyo aliamuru simu ziingie chaji bila kuchomekwa kwenye umeme.

Hivi sasa kumekuwa na wimbi kubwa la wachungaji ambao wamekuwa wakifanya matukio mbalimbali kwa waumini wao wakiita miujiza, ikiwemo kuwanywesha jiki waumini, kuchapisha nguo za ndani zilizo na sura zao, kuwaogesha pamoja na mambo mengine.