Jumatano , 14th Feb , 2024

Yang Binglin, ambaye pia anafahamika kama ''zee la magemu'' (Gamer Grandpa)anashikilia rekodi ya kuwa mcheza magemu wa mtandaoni ambaye ni mzee zaidi akiwa na umri wa miaka 88.

 

Alianza na magemu ya kawaida ambayo wacheza magemu wengi huanza nayo hapa nazungumzia game kama vile ''Brick game'' ambayo wengi tulicheza tulivyokuwa wadogo, 

Baada ya hapo, Yang Binglin; aliendelea kucheza magemu mengine kama vile Tomb Raider, Resident Evil, Sniper na mengineyo.

Maktaba ya mzee huyu kwa sasa (playroom) inajumla ya magemu zaidi ya 500 ikijumuisha baadhi ya magemu ambayo yametoka kipindi cha hivi karibuni kama vile X-bOx, PS5 ambayo alipewa kama zawadi na mashabiki zake mtandaoni

Kama utakuwa ni mtu wa kufuatilia filamu basi utakuwa umekwisha itazama Family Plan (2023) ambayo ndani yake kuna muhusika anaitwa  Kyle ambaye nae ni mpenda magemu itafute utaelewa maisha ya Yang Binglin alivyokuwa akiwa kijana.