Jumanne , 18th Feb , 2025

Instagram kwa sasa inafanya majaribio ya kuweka ''Dislike Button'' kwenye upande wa comment, kitu ambacho kitamfanya mtumiaji wa mtandao huo kuweka wazi hisia zake kuhusiana na comment husika bila ya kuonesha utambulisho wake wala idadi ya watu ambao hawajapendezwa na comment husika.

Kupitia mtandao wake wa threads mkuu wa Instagram Bw. Adam Mosseri ameandika kwamba; Baadhi yenu mtakuwa mmeona kuwa tunafanya majaribio ya kuweka button mpya kwenye upande wa comment kwenye mtandao wa instagram, hii itawapa watu nafasi ya usiri ya kutoa ishara ya kwamba sijapendezwa na aina ya comment husika, na labda niweke sawa. Hakuna dislike hata moja ambayo itaonekana kwa idadi na pia hakuna ambaye atafahamu iwapo umebonyeza button ya dislike kwenye comment yake, lakini kwa idadi ya uwepo wa dislike kwenye comment husika itakuwa sababu ya comment kushushwa kwenye mtandao huo, ni matumaini yetu hii itapelekea uwepo wa comment rafiki kwenye mtandao wa Instagram.

Vipi kwa upande wako, unadhani hii itasaidia kupunguza idadi ya comment chafu/mbaya kwenye mtandao wa Instagram?