
Pole kama umekumbwa na hili usitafute tena mchawi nani, chapu kwa haraka fuata haya kujinasua kwenye hili uendelea kupata huduma.
Kabla ya kusonga ufungiaji wa account za WhatsApp upo kwenye mgawanyo wa zile ambazo zimefungiwa kwa muda, zipo zilizofungiwa kwa siku na zipo zilizofungiwa milele daima,
Sasa hizi ni hatua chache za kufuata ili kujinasua kwenye hili -
1. Ingia kwenye ''Google Chrome'' andika ''contact WhatsApp'' bonyeza ''link'' ya kwanza kabisa.
2. Nenda palipoandikwa ''Contact us"
3. Kwenye form iliyokuja baada ya hapo andika +255 kwenye ''country code'' chini yake andika namba ya simu iliyofungiwa.
4. Sehemu ya nne utaandika ''Email'' yako itakuhitaji kuthibitisha kwa kuandika tena.
5. Utachagua kifaa ambacho unatumia kwa ajili ya ''account'' yako ya WhatsApp mfano Simu, Kishkwambi au kompyuta.
6. Mwisho kabisa utapewa chaguo la kuandika maelezo kidogo ya kuomba ufunguliwe ''account'' yako, baada ya hapo utasubiri ujibiwe ndani ya saa 11 hadi 12 kwa njia ya Email.
NB: Hii ni njia moja wapo ya kuomba kurejeshewa ''account'' yako ya WhatsApp na kuhusu uhakika wa kurudi inategemea kwani zipo ambazo zimefungwa kabisa, na kuhusu saa hutofautiana pia.