Jumatatu , 5th Feb , 2024

Elimu haina mwisho ni msemo ambao hata aliyeuanzisha pengine hatumfahamu, lakini ule usemi wa lisemwalo lipo kama halipo laja unaweza kuwa shuhuda kwenye hili,

 
David Marjot anaandika historia ya kuwa mhitimu mwenye umri mkubwa zaidi kwenye ngazi ya chuo kikuu, kutokea nchini Uingereza.

David Marjot ambaye ni daktari mstaafu kwenye maswala ya afya ya akili, ameandika historia hiyo baada ya kuhitimu shahada ya uzamili kwenye maswala ya Falsafa ya Kisasa, akiwa na miaka 95

''Shahada yangu haikuwa rahisi ilikuwa ngumu kwani kumbukumbu zangu hazikuwa kama nilivyokuwa zamani'' alisema David Marjot

Lakini Dk Marjot, kutoka Surrey, uingereza anafikiria kuchukua kozi nyingine ambayo atasonga nayo mpaka atakapofika miaka 102

Picha: BBC