Jumatatu , 2nd Jan , 2023

Elon Musk alikuwa mtu wa pili kuwahi kujikusanyia utajiri wa zaidi ya bilioni 200 akivunja rekodi ya kiwango hicho Januari 2021, miezi kadhaa baada ya Jeff Bezos. Sasa Elon Musk amekuwa binadamu wa kwanza kupata hasara ya dola bilioni 200 katika utajiri wake.

Mfanyabiashara Elon Musk.

Kulingana na mtandao wa Bloomberg, Musk (51) ameona utajiri wake ukishuka hadi dola bilioni 137 baada ya hisa za Tesla kushuka katika wiki za hivi karibuni ikiwamo kushuka kwa hisa 11% Jumanne ya wiki iliyopita.

Elon Musk alibakia kuwa mtu tajiri zaidi ulimwenguni kwa utajiri uliofikia dola bilioni 340 mnamo Novemba 4, 2021 mpaka alipopinduliwa na tajiri wa Ufaransa Bernard Arnault mwezi Disemba.