Jumatatu , 16th Mei , 2022

Johanna Mazibuko kutokea Afrika Kusini kwa sasa anatwaja ndiyo binadamu mzee zaidi Duniani akiwa na umri wa miaka 128.

Johanna anataka kitabu cha rekodi cha Guinness kitambue rekodi yake

Katika siku yake ya kuzaliwa Johanna alionesha cheti chake cha kuzaliwa ambacho kinaonesha alizaliwa mwaka 1894. Johanne ana wajukuu 50 na amebakiwa na watoto wawili waliohai katika ya saba aliozaa.

 

Guinness bado hawajatambua rekodi yake, mpaka sasa wanamtaja Lucile Randon ndio binadamu mzee zaidi akiwa na umri wa miaka 118.