Alhamisi , 14th Oct , 2021

Polisi nchini Nigeria wanamshikilia Godwin Matthew (26) kwa tuhuma za kumuuwa baba yake, Matthew Audu (64) baada ya kula nyama ya kuku yote kisha kumbakishia kichwa mwanae huyo.

Picha ya Godwin Matthew

Afisa Uhusiano wa Polisi katika jimbo la Ondo, DSP Funmi Odunlami amethibitisha tukio hilo la mauaji liliripotiwa katika kituo cha Polisi cha Ala na mke wa marehemu baada ya Godwin kutekeleza tukio hilo wakiwa shambani.