Ijumaa , 25th Apr , 2025

Chuo kikuu cha Stanford kutokea California, kimetengeneza mfumo wa akili unde ambao moja kwa moja utaenda kumsaidia mwanafunzi ambaye anapata tabu kwenye kukamilisha tafiti yake kutokana na uhaba wa maandiko na maelezo kuhusu mada husika.

Akili unde hii inaitwa ''Storm'' namna ya kuipata utaandika hivi ''https://storm.genie.stanford.edu/ ''

Utofauti wa STORM na akili unde nyingine
- Inakupa taarifa kulingana na wakati halisia kwani hupita kwenye kila kona ya mtandao kutafuta jibu na maelezo kuhusu mada husika.
- Uwezo mzuri wa kujibu mada yako kwenye mfumo wa tafiti (Research) na wenye kuvutia
- Inakupa marejeleo (references) kutoka sehemu sahihi
- Taarifa za kina zilizojaa uchambuzi makini

Kama unahitaji uchambuzi wa taarifa kwa kina, vyanzo halisia na mpangilio wenye kubeba maana basi tumia STORM A.I lakini kama unataka mawazo mapya ya haraka ambayo si marefu basi wewe tumia zako ChatGPT