Alhamisi , 20th Jun , 2024

Ilikuwa ni jioni nzuri na ya kupendeza kwa ajili ya chakula cha jioni, lakini iligeuka kuwa jioni ya mshangao na furaha isiyotegemewa.

Mwanamke mmoja huko North Little Rock, nchini Marekani aliyefahamika kwa jina la Tayvia Woodfork, alijifungua bila kutarajia alipokuwa msalani kwenye mgahawa maarufu wa Golden Corral uliyopo North Little Rock jambo ambalo binafsi yake anasema hakuwahi kufahamu kama yeye ni mjamzito.

Uzazi huu umeshangaza watu wengi mitandaoni kwani Tayvia mwenyewe amenukuliwa akisema hakuwahi kuona dalili zozote za yeye kuwa mjamzito ila alishangaa tu ghafla akiwa msalani alipata uchungu na kujifungua mtoto wa kiume.

Chanzo: Fox News