
Nyumba iliyochomwa moto
Mwanamke huyo amechoma moto nyumba hiyo kwa hasira, baada ya Mumewe Dominic Miti kumpa mke mwenzie pesa za Kenya Ksh 1000, za sikukuu ya Christmas huku yeye akiachwa mtupu .
Akizungumza na chombo kimoja cha habari nchini humo Mume wa wanawake hao Dominic Miti amesema, alijaribu kumsihi Mkewe awe mtulivu na kumpa siku kadhaa za kutafuta hela za kumnunulia bidhaa za sikukuu, lakini mkewe hakusikia.
"Nilikuwa napanga kumpa KSh 1,000. Hata hivyo hakutaka kuwa mtulivu" amesema Dominic Miti
Mwanaume huyo na mkewe walikamatwa na kufikishwa katika Kituo cha Polisi, lakini mume huyo aliachiwa siku moja.
Source, Tuko News