Jumanne , 8th Apr , 2014

Kundi la kipekee linalofanya muziki wa Hip Hop kutoka Zanzibar Zee Town Souljas linaloundwa na wasanii Kira Kirami pamoja na King Pozza, limewataka wadau wa burudani na mashabiki kujipanga kuhusu mpango wa kufanya ziara kubwa ya kimuziki Zanzibar.

Kira Kirami kutoka Zee Town Souljas

Wasanii hawa wameiambia eNewz kuwa, ziara hii itakuwa ni kwa ajili ya lengo kubwa la kuwaelimisha zaidi vijana juu ya athari za dawa za kulevya na kupiga vita ngono zembe kwa ajili ya kupunguza zaidi maambukizi ya virusi vya UKIMWI.

Zee Town Souljas pia wamewataka watanzania kupokea kazi zao na kupata ladha mpya ya Hip Hop kutoka Tanzania visiwani ambayo imezoeleka kwa kuzalisha muziki wa mwambao zaidi, maarufu kama Taarab.