Gari aina ya Toyota Vits ambayo itatolewa kama zawadi kwa mshindi wa shindano la urembo la Miss Tanga
Shindano kubwa la kuwania taji la ulimbwende mkoani Tanga linalodhaminiwa na kituo bora cha matangazo cha EATV limezidi kushika kasi baada ya gari dogo la mshindi wa Nice & Lovely Miss Tanga 2014 aina ya Toyota Vits kuwasili mkoani humo.
Mratibu wa shindano hilo Benson Jackson amesema kinyang'anyiro hicho kitakachofanyika Juni 21 mwaka huu mshindi wa shindano hilo atawakilisha mkoa wa Tanga katika mashindano ya ulimbwende kanda ya kaskazini kisha baadae kuwania taji la miss Tanzania.
Kwa upande wake mkufunzi wa miss Tanga Mariam Bandawe amewataka washiriki kujitokeza kuchukua fomu kwa ajili ya kinyang'anyiro hicho ambapo lengo hasa ni kutaka kumpata mshindi atakayefanya vyema katika mashindano hayo ngazi ya kanda na nchi nzima kwa ujumla.