Jumanne , 25th Nov , 2014

Staa wa muziki kutoka Kenya, Wyre The Love Child amefurahishwa sana na ushirikiano ambao wasanii wa muziki hapa Tanzania wanao katika kufanya kazi zao, akitolea mfano project ya Embe Dodo ya msanii wake Bee Man.

msanii wa nchini Wyre akiwa na msanii wake Bee Man

wyre amesema kuwa hii ni moja ya project kubwa ya Bee Man ambayo imekutanisha pamoja wasanii saba wakali wa kuimba hapa Bongo.

Wyre ambaye amekwishafanikiwa kuingiza muziki wake katika anga za kimataifa, amesema kuwa, kwa ushirikiano wa namna hii katika kazi anaamini kuwa kazi hii pamoja na muziki wa Afrika Mashariki kwa ujumla utafika mbali zaidi.