Jumamosi , 9th Jan , 2016

Nyota wa muziki Witnesz, pembeni ya game yake ya muziki, kama njia mojawapo ya kurudisha fadhila kwa jamii ambayo inajumuisha mashabiki wake, anaendesha mradi wa kupambana na ndoa za utotoni akishirikiana kwa karibu na msanii na mpenzi wake, Ochu.

Wintesz

Witnesz, kupitia mahojiano aliyofanya na eNewz ameeleza kuwa, project hiyo ambayo itahusisha pia rekodi ya muziki, itagusia haki za msingi za watoto wa kike wanaolazimishwa kuolewa, ikiwepo elimu na uhuru wa kujichagulia mwenza wa maisha.

Msanii huyo amesema kuwa, pindi video ya kazi hiyo itakapokamilika ataiachia rasmi mtandaoni kupitia chanel yake mpya You Tube Witneszkibongemwepec kwaajili ya mashabiki kujifunza na kuburudika.