
mmoja alizofanya.
Baraka Da Prince ameyasema hayo kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, na kueleza kwamba kwa sasa wanajipanga kwenda kufanya video ya wimbo huo nchini Afrika Kusini, ambayo itaifanya nyimbo hiyo kusikilizwa zaidi.
"Ni wimbo ambao unaenda vizuri upande wa Nairobi na East Africa, na ni nyimbo ambayo un aweza ukasema zilipokelewa vizuri, ile nyimbo haikukaziwa promotion kwa sababu iliambatana na nyimbo ambayo King Kaka alifanya na Richard Mavoko, sasa hii Plan yake ilikuwa tufanye video then ndo aikazie katia promotion", alisema Baraka.
Baraka Da Prince aliendelea kwa kusema kuwa siku za hivi karibuni wanatarajia kusafiri kuelekea nchini Afrika Kusini kufanya video ya wimbo huo.
"After one month nadhani tutasafiri kwenda South Africa, video tunaenda kufanyia South Africa alivyoniambia, kwa hiyo namsikilizia yeye kwa hiyo ni nyimbo ambayo bado iko kwenye plan na iko kwenye mipango mizuri kuindeleza ili iwe nyimbo kubwa", alisema Baraka Da Prince.