Jumanne , 28th Apr , 2015

Watoto wa aliyekuwa staa wa muziki wa nchini Uganda, Marehemu AK-47 chini ya uangalizi wa baba yao mkubwa, msanii wa muziki Pallaso pamoja na mama yao Maggie, wamebatizwa na kupatiwa majina Connie na Canaan huko nchini Uganda.

msanii wa nchini Uganda Pallaso akiwabeba mapacha wake AK-47

Tukio hilo limehudhuriwa na takriban watu 200, na Pallaso kukabidhiwa rasmi jukumu la kuwa nao karibu zaidi kama baba mlezi, na kuhakikisha anawaongoza kimaadili katika misingi ya imani hiyo ya kikristo.

Mapacha hao walizaliwa mwezi Novemba mwaka Jana na kuondokewa na baba yao mzazi miezi minne baadaye, pigo kubwa ambalo bado familia yake inaendelea kupona maumivu yake mpaka sasa.