Jumamosi , 23rd Mei , 2015

Shughuli kubwa ya ugawaji wa tuzo kwa kazi na wasanii bora wa tasnia hiyo kupitia Tanzania Film Awards 2015, inafanyika leo na inatarajiwa kuanza majira ya saa mbili usiku Mwalimu Nyerere Conference Centre jijini Dar es Salaam.

Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) Simon Mwakifambwa

Tukio hili la kihistoria na la aina yake mbali na ugawaji tuzo litahusisha kwa uzito wake burudani za muziki kutoka kwa wasanii King Kikii, Barnaba, Mwasiti, na kwa upande wa vichekesho Oscar Nyerere pia vilevile Mrugaruga na vichekesho, vilevile likitarajia ugeni mkubwa wa wadau wa filamu kutoka nchi za Afrika Mashariki, Ghana, Nigeria na Marekani.

Tiketi kwaajili ya kuingia kutazama show hii zinapatikana kwa shilingi 50,000 kwa kawaida na 100,000 kwa VIP, na kwa chap chap tu fahamu unaweza kujipatia tiketi yako Shear Illussion - Mlimani City na Millenium Towers, Robby One Fashion- Kinondoni na Sinza Africasana, B&B Boutique- Dar Free Market duka namba 46 na Viva Towers duka namba 31, Secky Bureau de Change - Big Bon Sinza Mori, Save Mart wholesalers - Mikocheni kwa Nyerere EATV na ITV.

Mastaa kibao ndani, tukutane pale.