Wasanii waliotangazwa leo ni katika kipengele cha filamu bora ya mwaka na kipengele cha muigizaji bora wa kike.
Mkuu wa Matukio wa Baraza za Sanaa Tanzania (BASATA), Kurwijira Maregesi alitaja majina matano ya wasanii wanaowania kipengele cha muigizaji bora wa kike (na jina la filamu kwenye mabano) kuwa ni
Nominee: Chuchu Hansy (Laura)
Nominee: Khadija Ally (3 Days)
Nominee: Frida Kajala Masanja (Hii ni laana)
Nominee: Rachael Bitulo njingo (Nimekosea wapi)
Baada ya kutangazwa kwa washiriki hao katika kipengele cha muigizaji bora wa kike, mwakilishi kutoka Vodacom Tanzania, Ibrahim Kaude ambao ni wadhamini wakuu wa tuzo za EATV AWARDS kwa kushirikiana na Coca Cola aliweza kutaja majina matano ya wasanii wengine ambao wanawania tuzo katika kipengele cha filamu bora ya mwaka kama ifuatavyo.
Filamu iliyoingia- Safari ya gwalu
Filamu iliyoingia- Hii ni laana
Filamu iliyoingia- Mfadhili wangu
Filamu iliyoingia- Nimekosea wapi
Filamu iliyoingia- Facebook profile